Space X kuwasafirisha watalii 2 mwezini 2018.

MWEZIN

Kampuni ya kibinafsi ya kurusha roketi imetangaza kwamba watalii wawili wamelipa kupelekwa mwezini.

Safari hiyo itafanyika 2018 kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SpaceX Elon Musk, alieongezea kwamba watalii hao tayari wamelipa kiasi fulani cha fedha.

”Hatua hiyo inatoa fursa kwa binaadamu kurudi katika anga za juu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 45”,alisema.

Wawili hao ambao majina yao hayakutajwa wataelekea mwezini wakiwa katika meli hiyo ya angani ambayo itafanyiwa jaribio lake la kwanza la kurusha rekoti isiokuwa na rubani.

Bwana Musk alisema kuwa ushirikiano wa shirika la sayansi na teknolojia ya angani nchini Marekani Nasa umefanya ufanisi wa safari hiyo.

#SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments