Soko la Hisa Dar es salaam Limepanda

img-20161213-wa0030

Afisa Mwandamizi wa Soko la Hisa Dar es salaam Bi. Mary Kinabo

Imeelezwa kuwa mauzo yamepanda mara sita zaidi kutoka shilingi za kitanzania milioni 198 wiki iliyopita hadi kufikia shilingi bilioni 1.22 kwa wiki iliyoishia tarehe tisa Desemba.
Hayo yameelezwa na Afisa mwandamizi wa soko la hisa jijini Dar es salaam Bi.Mary Kinabo ambapo amesema idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa katika wiki iliyopita imeongezeka kwa asilimia 44 kutoka hisa 262,598 kwa wiki iliyopita hadi hisa 378,149 kwa wiki hii.
Afisa Kinabo amesema ukubwa wa mtaji wa makampuni ulishuka kwa asilimia 0.5 kwa makampuni ya ndani umeendelea kubaki katika kiwango kilekile cha Trilioni 8 wakati viashiria sekta ya viwanda imeshuka kwa pointi 104.63,sekta za huduma za kibenki na kifedha imeshuka kwa pointi 3.66.
Amesema sekta ya huduma za kibiashara kwa wiki hii imeendelea kubaki kwenye wastani uleule wa shilingi za kitanzania 3,157/= sawa na wiki iliyopita.

#SIBUKA MEDIA

#Imeandaliwa na Tuse Kasambala

Comments

comments