Sita wasakwa kwa mauaji na wizi

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ulrich Matei amesema tukio hilo lilitokea Aprili 30, mwaka huu, saa tatu usiku, pale majambazi hayo yalivamia duka la Derigo Joseph kwa lengo la kuiba na ndipo yalipofyatua risasi.

Morogoro. Polisi mkoani Morogoro inawasaka watu sita kwa tuhuma za kufyatua risasi iliyosababisha kifo cha Joseph Abubakar walipovamia duka alilokuwa ananunua mahitaji yake katika eneo la Mkundi katika Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ulrich Matei amesema tukio hilo lilitokea Aprili 30, mwaka huu, saa tatu usiku, pale majambazi hayo yalivamia duka la Derigo Joseph kwa lengo la kuiba na ndipo yalipofyatua risasi.

Amesema kwamba mwenye duka alifanikiwa kukimbia na risasi hizo kumpata mteja wake.

Kamanda huyo amesema kuwa Abubakar alifyatuliwa risasi ya puani ambayo ilitokea kwenye utosi na kusababisha kifo chake papo hapo.

“Majambazi hawa walifanikiwa kuiba simu sita za aina tofauti na fedha taslimu Sh133,000,” amesema Matei na kuongeza kuwa jeshi hilo bado linaendelea kuyasaka

Comments

comments