Simu ambazo hazifanyi kazi tena na WhatsApp

_93259621_a2cf29b0-1cc9-4a56-a5f8-f174f674c44e

Huduma ya WhatsApp haitumiki tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zinazotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6.

Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo ilisema inataka kuangazia kustawisha “huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi.”

WhatsApp, ilipangiwa kuacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu mwishoni mwa Desemba 2016.

Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka jana.

_93259624_93a8ff19-86bc-4596-b2fc-8152be6cccee

Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:

Android 2.1 na Android 2.2
Windows Phone 7
iPhone 3GS/iOS 6
Simu ambazo wateja wake hawataweza kutumia Whatsapp ifikapo Juni 30, 2017 ni:
BlackBerry OS and BlackBerry 10
Nokia S40
Nokia Symbian S60
Wanaotumia simu za aina hiyo wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi.
Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia.

Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.

#BBC SWAHILI

#SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments