Shule za Msingi mkoani Singida hatarini kupata magonjwa ya Milipuko.

SINGIDA

Imebainika kuwa Wanafunzi katika baadhi ya shule za Msingi zilizopo Wilayani Mkalama mkoani singida wapo hatarini kupata magonjwa ya Milipuko kutokana na huduma duni za upatikanaji wa maji salama katika shule hizo.

Afisa elimu Msingi Wilaya ya mkalama Bw,Chacha James Kehogo amethibitisha kuwepo kwa changamoto hiyo wakati alipokuwa akizungumza na sibuka fm ofisini kwake na kusema kuwa kuwa kutokana na hali hiyo inapelekea wanafunzi kutumia maji yasiyo salama kwa matumizi ya binadamu hivyo kuweza kupelekea magonjwa ya mlipuko kwa wanafunzi.

Hata hivyo  bw. Kehogo amesema kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo Halmashauri imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ambapo imeweza kuchimba visima katika maeneo mbalimbali licha ya kutotosheleza kwa shule zote lakini jitihada zinaendelea kuboresha huduma ya katika shule hizo.

  • Mwandishi : Saulo Steven
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments