Shirika la viwanda vidogo vidogo -SIDO- mkoa wa SINGIDA limetoa mafunzo ya ubora na usalama wa mafuta ya alizeti na bidhaa zake.

Shirika la viwanda vidogo vidogo -SIDO- mkoa wa SINGIDA kwa ushirikiano na shirika la TFDA na TBS, limetoa mafunzo ya ubora na usalama wa mafuta ya alizeti na bidhaa zake, kwa wasindikaji  25 wa tarafa ya SHELUI wilaya ya IRAMBA mkoa wa SINGIDA.

Lengo la mafunzo hayo,ni wasindikaji hao waweze kupata hati safi ya usindikaji wa mazao ya alizeti,itakayokubalika na shirika la TFDA na TBS.

Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo meneja  wa SIDO mkoani SINGIDA, SHOMA KIBENDE amesema mafunzo hayo   yatawasaidia kwa kiasi kukubwa wasindikaji hao kumudu ushindani wa kibiashara uliopo.

Mkuu wa wilaya ya IRAMBA,EMMANEUL LUHAHULA,amelipongeza shirika la SIDO kwa uamuzi wake wa kutoa mafunzo hayo kwa wamiliki na wawakilishi wa viwanda vidogo  na vikundi vinavyo kamua mafuta ya alizeti.

Katika hatua nyingine,mkuu huyo wa wilaya,amemwangiza mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya wilaya ya IRAMBA,kuhakikisha viwanda vidogo ya kusindika mafuta ya alizeti,vinakuwa na maji ya kutosha kwenye viwanda hivyo wakati wote.

Mmoja wa wasindikaji hao,YASINI MBOLOLE amesema mafunzo hayo kwa kiasi kikubwa yatawasaidia kuondokana na usindikaji wa mazoea,na sasa  wataongeza ubunifu utakaosaidia kazi zao zikubalike na shirika la TFDA na TBS.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments