Shirika la jukwaa la utu wa mtoto(CDF) kwa kushirikiana na halmashauri ya manispaa ya Ilala

IMG_0863

Shirika la jukwaa la utu wa mtoto(CDF) kwa kushirikiana na halmashauri ya manispaa ya Ilala wamefanya mkutano wa mrejesho wa mradi wa kuhamasisha jamii kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Kitunda.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa shirika la jukwaa la utu wa mtoto (CDF) Bw.KOSHUMA MTENGETI amesema mkutano huo umelenga kuhamasisha jamii kutokomeza ukatili unaosababisha na mimba za utotoni, ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji.

IMG_0860

MTENGETI amesema takwimu za CDF  zinaonyesha   vitendo vya ukatili wa kijinsia katika ukeketaji bado vipo juu ambapo mwaka 2010 ilikuwa ni asilimia 15 na mwaka 2016 imepungua mpaka asilimia 10 na kusisitiza kuwa mikoa  ya Singida Mara,Dodoma na Manyara takwimu bado iko juu.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya maendeleo ya watoto na ustawi wa jamii Ilala Bi.JOYCE MAKETA amesema manispaa ya Ilala inaendelea kushirikiana na CDF katika kutekeleza miradi ya kupinga ukatili lengo ni kuhakikisha ukatili unatokomezwa katika manispaa hiyo.

Hata hivyo amesema jamii ikipewa elimu ya afya ya uzazi mara kwa mara itasaidia kwa kiasi kikubwa kutokomeza ukatili wa kijinsia

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments