Serikalini Inatarajiwa kutangaza zabuni ya vifaa siku ya tarehe 27 mwezi wa pili mwaka 2017/18

IMG-20170216-WA0001

Wakala wa ununuzi serikalini  unatarajiwa kutangaza zabuni ya vifaa siku ya tarehe 27 mwezi wa pili mwaka 2017/18 ambapo mikataba yote ya uzabuni ya serikari itapitishwa na wakala huo mara baada ya kuhakikisha vigezo vya zabuni husika vina sifa ya kupata zabuni hiyo.

IMG-20170216-WA0002

Amesema hayo leo katibu mtendaji wa wakala wa huduma wa serikala GPSI Bw. Jacob Kibona kuwa  siku hiyo wakala utatangaza zabuni ya vifaa na huduma kwa watakaotaka kufanya huduma na taasisi za umma kwa mwaka mmoja wa faedha  2017/2018 na kutakuwa na aina 25 za uzabuni ambapo 12 ni za vifaa na 13 ni za huduma mbalimbali ambapo mikataba yote iakayotolewa  itakuwa ni yam waka mmoja.

Ameongeza Bw. Kibona kusema kuwa mikataba ya huduma na vifaa hivyo haitakuwa na bei kwa mujibu wa marekebisho ya sharia ya mwaka 2016 tozo asilimia mbili kwa kila muamala haitokuwepo na badala yake kiasi cha shilingi laki moja tu kitalipwa mara moja kwa mwaka kwa kila mkataba maalum wa kufanya kazi na taasisi za serikali.

Amebainisha kuwa  wakala kwasasa hautatoa wala kutangaza zabuni kwajili ya huduma kama ulinzi,kumbi za mikutano, upatikanaji wa tiketi kwa usafiri wa ndege na hoteli na kueleza kuwa huduma hizo zitakuwa zikishughulikiwa na taasisi husika moja kwa moja.

IMG-20170216-WA0003

Mikataba ya uzabuni wa vifaa na huduma wa serikali nchini ilitolewa  na kutumika hadi sasa ni yam waka 2014/15 ambayo ni ya miaka mitatu 2015/16 ya miaka miwili na 2016/17 ambayo itamalizika ifikapo mwezi juni 30 2017

Imeandaliwa na Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments