Serikali ya Italia imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania.

ITALIA

Serikali ya Italia imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kuboresha hali ya maisha ya wananchi na kupunguza vifo vya watoto kupitia njia ya maji na lishe .

Serikali hiyo ya Italia imezindua mradi wa Maishani  Maji na Lishe huku zaidi ya shilingi Trilioni 2.9 zikitaraji kutumika katika mradi huo kwa awamu ya kwanza katika mikoa ya Dodoma na Iringa.

Uzinduzi wa mradi wa Maji na lishe umefanyika kitaifa mkoani Dodoma na unatajwa kuwa chachu ya kupunguza vifo vitokanavyo na udumavu pamoja na kuondokana na tatizo la maji.

Roberto Mengoni ni Balozi wa Italia nchini Tanzania akizungumza na washiriki katika uzinduzi wa mradi huo amesema ni dhamira ya serikali ya Italia katika kusukuma juhudi za maendeleo nchini Tanzania na kwamba anataraji mradi huo utaleta manufaa katika utekelezaji wa awamu ya kwanza

Akitoa salamu za serikali ya Tanzania Katibu Tawala mkoa wa Dodoma Rehema Madenge akatoa maagizo kwa wasimamizi wa miradi inayotekelezwa kuhakikisha wanawashirikisha wananchi katika miradi hiyo.

Elias Mtagwa Mkazi wa Kongwa  wa washiriki wa washiriki katika uzinduzi wa mradi huo wamesema kuwa katika maeneo yao hasa ya vijijini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya lishe bora pamoja na ukosefu wa huduma ya maji hivyo.

Kwa upande wake Mhandisi Mathayo Athumani ambaye ni Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Maji mkoani Dodoma amesema kuwa asilimia kubwa ya magonjwa yanatokana na kutozingatia Lishe Bora pamoja na kutotumia maji safi na salama

Ili kuondokana na tatizo la lishe bora pamoja na matumizi ya maji safi na salama mwito unatolewa kwa serikali na wadau wa maendeleo kutoa elimu juu ya matumizi ya maji safi na salama sambamba na lishe bora itakayosaidia kupunguza vifo katika maeneo mbalimbali nchini.

  • Mwandishi :Barnaba Kisengi.
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts