Serikali kupitia wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali

Mkemia Mkuu

Mkemia mkuu wa serikali Profesa Manyele

Serikali kupitia wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali imenunua mtambo mpya na wa kisasa wa uitwao Energe Disperive XrayFluorescence (EDXRF) ambao utatumika uchunguzi wa kimaabara wa kutambua aina ya madini na kiasi cha madini kwenye sampuli husika.

Amesema hayo leo jijini Dar es salaam mkemia mkuu wa serikali Profesa.Samweli Manyele kuwa mtambo huo utaanza kufanya kazi katika jiji la mbeya ambapo utasaidia pia kurahisisha kutambua  madini yalipo ,kulinda afya za watu na mazingira dhidi ya madhara ya kemikali na sheria ya vinasaba vya binadamu sura namba 73 yenye lengo la kudhibiti teknolojia ya vinasaba hapa nchini.

Amebainisha kuwa mtambo huo wa kisasa mbali ya hayo utatumika kuchunguza makosa ya jinai kama dawa za kulevya,sampuli za sumu na nyinginezo ili kutoa majibu yanayowezesha utoaji wa haki katika vyombo vya sheria.

Aidha mkemia mkuu  profesa Manyele amesema kuwa mtambo huo umegharimu  shilingi za kitanzania mia moja na moja milioni ,mia saba themanini na tano elfu na mia mbili sawa na dola za kimarekani 46,266

Imeandaliwa na Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments