Serikali imewasilisha bungeni Muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali .

bungeT

Serikali imewasilisha bungeni Muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali unaolenga kufanya marekebisho yatakayorahisisha utekelezaji wa sheria ambapo muswada umebainisha kutoza faini ya shilingi milioni 5 au kifungo cha miaka sita kwa mkuu wa taasisi za umma atakayeingia mkopo pasipo kupata kibali cha waziri wa Fedha.

Ni Bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania mkutano wa sita hapa mjini  Dodoma ambapo pamoja na shughuli nyingine bunge linapokea taarifa ya Muswada wa sheria ya marekebisho mbalimbali ya mwaka 2016 na wabunge kuanza kuchangia

Akiwasilisha muswada huo Mwanasheria mkuu wa serikali George Masaju amesema kuwa kupitia muswada huo utawezesha mkopo uliochukuliwa kwa dhamana ya serikali utatumika kwa kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo

George Masaju Mwanasheria mkuu wa serikali

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya katiba na sheria Mohamed Mchengerwa amesema kupitia muswada huo utawezesha kuboresha huduma za msaada wa kisheria

Mohamed Mchengerwa Mwenyekiti kamati…….Msemaji wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Katiba na Sheria Tundu Lissu naye akatoa maoni ya kambi ya upinzani juu ya Muswada huo

 Tundu Lissu Msemaji kambi ya Upinzani Katiba na sheria

Wabunge bado wanaendelea na majadiliano pamoja na kupokea taarifa pamoja na miswada mbalimbali hapa bungeni mjini Dodoma

Imeandaliwa na Barnaba Kisengi

#SBUKAMEDIA

Comments

comments