Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 605 za nyongeza katika bajeti kwa mwaka wa fedha 2017/18

u

Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 605 za nyongeza katika bajeti kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwa ajili ya watumishi waliopandishwa na wanaotarajiwa kupandishwa madaraja pamoja na ongezeko la mshahara.

Hayo yamesemwa leo jijini DAR ES SALAAM na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala bora BI.ANGELA KAIRUKI katika semina elekezi ya watumishi wa umma waliopandishwa  na wenye barua za kupandishwa vyeo lakini wakasitishiwa kutokana na uhakiki wa vyeti.

Waziri KAIRUKI amesema fedha hizo pia zitalipa malimbikizo ya mishahara pamoja na kutekeleza suala zima la ajira mpya.

uu

Aidha waziri amewaagiza waajiri kuajiri watu waliohakikiwa ili kuepusha kuajiri watumishi wasiokidhi vigezo ikiwemo wenye vyeti feki kwani kufanya hivyo kutaathiri utendaji kazi.

Waziri KAIRUKI amesema kuwa tayari serikali imetoa kibali cha kuajiri watumishi 10,184 kwaajili ya kuziba pengo la watumishi walioondolewa baada ya kugundulika na vyeti feki.

  • Mwandishi Tuse Kasambala.
  • SIBUKA MEDIA

Comments

comments