Serikali imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya watumishi wenye kughushi vyeti pamoja na watumishi hewa ambao walikuwa wakiendelea kupokea mshahara.

oo

DAR ES SALAAM:

Serikali imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya watumishi  wenye kughushi vyeti pamoja na watumishi hewa ambao walikuwa wakiendelea kupokea mshahara.

Changamoto hiyo imetolewa  leo jijini Dar es salaam na Waziri nchi Ofisi ya Rais Menejimenti   ya utumishi wa Umma  na utawala bora  Mh. Angela  Kairuki wakati  akizungumza  na watumishi wa umma wa wilaya Kinondoni na kueleza kuwa baadhi ya watumishi waliokuwa wakilipwa walishafariki na wengine  tayari ni wastaafu pamoja na wasio na vyeti halali.

Waziri Kairuki  amesema kuwa uhakiki wa vyeti umekuwa ukifanywa kwa umakini mkubwa kupitia mfumo wa kanzidata kwa kushirikiana na RITA na TRA.

Aidha amewataka watumishi wa umma kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi kwa mujibu wa sheria na kuzingatia maadili ya kazi.

Pia ametoa angalizo kwa   watumishi wa umma wanaotumia vibaya matumizi ya taarifa ya serikali kwa njia ya mtandao kuacha mara moja vinginevyo wakibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Amebainisha kuwa jumla ya watumishi elfu kumi mia moja na themanini na nne wanatarajia kupata ajira serikalini.

Ametoa wito kwa watumishi wa umma kubadili mfumo wa maisha yao ili kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi na mengineyo yanayoambukiza sambamba na kufanya mazoezi ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na presha.

o

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amezitaja changamoto zinazoikabili wilaya ya Kinondoni kuwa ni upungufu wa watumishi katika idara ya Ardhi ambao wako nane tu hivyo amemuomba Waziri Kairuki kushughulikia suala hilo ili kurahisisha utendaji kazi katika wilaya hiyo sambamba na kusema kuwa jumla ya watumishi 144 wa sekta ya afya katika wilaya yake wamekutwa na vyeti feki.

Waziri Kairuki tayari amefanya ziara katika wilaya ya Temeke,Mbagala,Kigamboni na sasa Kinondoni ili kuzungumza na watumishi wa umma

 

 

 

Comments

comments