Serikali imepitisha sheria mpya ya madini nchini.

Serikali imefuta wakala wa ukaguzi wa madini  na kuanzisha tume ya madini ambayo itasimamia shughuli zote za madini.

 Hatua imefikiwa baada ya kupitishwa sheria mpya ya madini ijulikanayo kama THE WRITTEN LAWS iliyoanza kutumika tarehe 7,Julai,2017 baada ya kufanyika kwa marekebisho kadhaa katika sheria ya madini ya mwaka 2010.

 Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Profesa JAMES MDOE wakati akizungumzia mabadiliko hayo jijini DAR ES SALAAM.

 Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu  Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe kuwa mabadiliko hayo ni kuanzishwa kwa sheria ya madini,kufutwa kwa wakala wa ukaguzi wa madini (TMAA) pamoja na kuongezeka kwa malipo ya mrabaha kutoka 4% kwa madini ya metali hadi kufikia 6%.

 Aidha Profesa MDOE amesema kupitia marekebisho ya sheria ya fedha  ya kodi hivi sasa kila mtu au kampuni anayetaka kusafirisha madini nje ya nchi yatakaguliwa  na kuthaminishwa  na muhusika kulipia ada ya ukaguzi (Clearing Fees)  ambayo ni asilimia 1 ya thamani ya madini anayosafirisha.

  • Mwandishi : Tuse Kasambala
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments