Semenya ashinda dhahabu mbio za 800m, Niyonsaba wa Burundi ashinda fedha.

Semenya

Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya alishinda dhahabu katika mbio za 800m upande wa wanawake siku ya mwisho ya mashindano ya ubingwa wa riadha duniani jijini London.

Bingwa huyo wa Olimpiki aliandikisha muda wa dakika moja na sekunde 55.16, muda wake bora zaidi na muda bora zaidi duniani mwaka huu.

Francine Niyonsaba wa Burundi alishinda fedha naye Ajee Wilson wa Marekani akachukua nishani ya shaba, wote wawili wakizidiwa na kasi ya kushangaza ya Semenya mita 50 za mwisho katika mbio hizo.

Mkenya Margaret Nyairera Wambui alimaliza wa nne.

  • #BBC SWAHILI
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments