SEHEMU ya jengo la kituo cha Clouds Media Group limeungua moto.

clouds

SEHEMU  ya jengo la kituo cha Clouds Media Group lililoko Mikocheni jijini Dar es Salaam limeungua moto leo majira ya asubuhi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo hicho, RUGE MUTAHABA, moto huo ulianzia studio ndogo ya kurekodia pasipo kujua nini chanzo.

RUGE amesema hii si mara ya kwanza moto kuteketeza baadhi ya vifaa vya studio kwani mara ya kwanza janga la moto lilitokea wakati wako jingo la Kitega uchumi ,posta hapa jijini DAR ES SALAAM na kuteketeza studio.

Mpaka sasa hakuna binadamu aliyepata madhara kwa kuwa kikosi cha zimamoto kiliwahi kufika eneo la tukio na kuzima moto huo kwa haraka.

  • SIBUKAMEDIA

 

 

 

 

 

 

Comments

comments