Scott Morrison ni waziri mkuu mpya Australia baada ya Malcom Turnbull kutimuliwa

Scott Morrison anatarajiwa kuwa waziri mkuu mpya wa Australia baada ya Malcom Turnbull kutimuliwa kwa lazima na chama chake maafisa wamethibitisha.

Turnbull alikuwa kwenye shinikizo kubwa kuanzia kuorodheswha chini katika kura za kutafuta maoni, uchaguzi unaowadia, na kugeukiwa na wabunge wa kihafidhina.

Morrison ambaye ndiye mweka hazina wa sasa alishinda kura 45 kati ya 50 ya ndani dhidi ya waziri wa mambo ya ndani Peter Dutton amaesema kinara wa chama cha kiliberali Nola Maroni.

Turnbull hakuwania katika ushindani huo wa uongozi.

Alikubali kuandaa kura baada ya idadi kubwa ya wabunge katika chama chake kusaini barua kutaka uchaguzi ufanyike.

Turnbull alikuwa akipuuzia wito wa kumtaka ajiuzulu wakati tuhuma za uongozi zikiididimiza serikali yake.

Jana Alhamisi , aliwaambia waandishi habari, kuwa raia nchini Australia ‘watashangazwa mno kwa wanachokishuhudia’.

Waziri wa mambo ya nje Julie Bishop pia ni miongoni mwa waliogombea nafasi hiyo, lakini hakufanikiwa katika duru ya mwisho.

Bwana Turnbull na Bi Bishop hawakuzungumza na waandishi habari moja kwa moja baada ya kura hiyo.

Kutoka kushoto hadi kulia: Malcolm Turnbull, Peter Dutton, Scott Morrison, Julie Bishop

Waziri mkuu mpya Morrison ni nani?

Morrison aliwahi kuwa mkurugenzi msimamizo wa utalii Autralia ambaye ameshikilia wizara kadhaa zikiwemo za uhamiaji na huduma kwa jamii.

Mhafidhina anayewavutia wanachama wa wastani ndani ya chama cha Kiberali.

Alipata umaarufu kitaifa alipokuwa waziri wa uhamiaji katika serikali ya waziri mkuu wa zamani Tony Abbott.

Alijenga sifa ya kuwa kiongozi asiyetaka upuuzi katika kuidhinisha sera kali ya Australi ya kusitisha uhamiaji.

Alikabiliwa na shutuma kuhusu sera zilizokumbwa na mzozo wa vituo vya kuomba hifadhi na kuwazuia wahamiaji.

Anatazamwa kama mwanasiasa mwenye azma jkuu ambaye kwa muda mrefu ametaka kuwa katika wadhifa huo mkuu.

Kiongozi huyo mwenye miaka 50 ni baba wa watoto wawili na mhafidhina wa dini anayepinga ndoa za jinsia moja.

Turnbull na Morrison
Image captionTurnbull na Morrison

Ni kwanini siasa za Australia zina mtikisiko mkubwa?

Muongo mmoja uliopita siasa nchini Australia zimekumbwa na msururu wa viongozi kutimuliwa, huku mawaziri wengine wakuu watatu wakitimuliwa na wapinzani wa chama.

Hakuna hata kiongozi mmoja katika siku za hivi karibuni amefanikiwa kuhudumu kwa muhula mzima wa miaka mitatu kama waziri mkuu nchini.

Chini ya mfumo wa Australia, waziri mkuu hachaguliwi moja kwa moja na wapiga kura, lakini ndiye kiongozi wa chama au muungano unaoweza kuwa na uwingi bungeni.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni, mawaziri wakuu ambao hawana umaarufu katika kura za kutafuta maoni, au miongoni mwa viongozi wenzake, wamekuwa wakitemwa kutoka ndani ya chama

Comments

comments