Sakata la uwekezaji katika bwawa la Katosho lililopo manispaa ya kigoma Ujiji .

KIGOMA

Kufuatia kuwepo kwa sakata la uwekezaji katika bwawa la katosho lililopo manispaa ya kigoma ujiji ,wakazi wa kahabwa na butunga, wameiomba serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuingilia kati suala hilo sambamba na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo kutoa majibu juu ya umwagaji wa sumu katika bwawa hilo.

hatua hiyo imekuja kufuatia agizo lililotolewa na mkuu wa wilaya ya kigoma Samson Anga mnamo februali 17 mwaka huu kwa kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuacha kuyatumia maji ya bwawa hilo  ili kupisha uchunguzi ufanyike kutokana na madai ya kuwepo kwa sumu ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu.

wakizungumza na sibuka fm wakazi hao wamesema kufuatia  kuchelewa kwa majibu juu ya uchunguzi huo imepelekea adha kubwa kutokana na shida ya maji wanayoipata kutokana na awali kutegemea zaidi maji ya bwawa hilo lakini kwa sasa hali imekuwa ni tofauti kwa kushindwa kuyatumia maji hayo kwa kuhofia usalama wa maisha yao.

Aidha akijibu tuhuma hizo mkuu wa wilaya hiyo Samson Anga amesema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mkemia wa serikali  tayari uchunguzi juu ya maji hayo umeshakamilika  na majibu yanatarajiwa kumfikia ndani ya kipindi cha wiki moja kutoka sasa na hivyo kuwataka wakazi hao kuwa watulivu na wavumilivu wakati wakisubiri majibu yaweze kutolewa na kufahamu mustakabari wa matumizi ya maji katika bwawa hilo.

  • Mwandishi : Saulo Stephen.
  • #SIBUKAMEDIA.

Comments

comments