Real Madrid Kuinuka Mshindi kwa mabao 4 kwa 1 dhidi ya washindani wao Juventus.

IMG-20170605-WA0015

Michuano ya UEFA Champion ligi 2017 imemalizika kwa timu ya Real Madrid kuibuka mshindi kwa mabao 4 kwa 1 dhidi ya washindani wao wa timu yaJuventus.

IMG_20170605_085821_086

Katika kuhakikisha mashabiki wa UEFA ligi wanashuhudia fainali hiyo Heinkein Tanzania wamejumuika na mashabiki wake  pamoja na vyombo vya habari katika kushuhudia mtanange huo huku wakiburudika na kinywaji bora duniani cha Heinkein.

Akizungumza afisa uhusiano wa kampuni ya bia ya Heinkein Bw. Bethuel Kinyori amesema kwa kutambua mchango wao pamoja na kutokana na wao kuwa ndio wafadhili wakuu wa michuano ya uefa 2017 wameona ipo haja ya kuwakutanisha wadau na mashabiki ili kuweza kushuhudia fainali hiyo.

 IMG-20170605-WA0010

Katika fainali hiyo mabingwa wa kihistoria wa kombe hilo  timu ya Real Madrid iliibuka na ushindi wa wa magoli 4 kwa moja dhidi ya juventus.

Kufuatia ushindi huo timu ya real Madrid inaendelea kushikilia rekodi ya kuwa timu ambayo imechukua kombe hilo mara nyingi zaidi katika historia ya michuano hiyo tangu kuanza.

Kwa upande wa mashabiki na wadau wa Heineken Tanzania wametoa pongezi kwa viongozi wa kampuni hiyo kwa kutambua na kuwakutanisha kuweza kushuhudia fainali hizo.

Mwandishi : Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments