Rais YOWERI KAGUTA MUSEVENI wa UGANDA Awa mshindi tuzo ya ukombozi Afrika

Museveni

Kamati inayoratibu Tuzo ya Ukombozi Afrika imemteua Rais YOWERI KAGUTA MUSEVENI wa UGANDA kuwa mshindi wa Tuzo hiyo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo DK.GEORGE NANGALE amesema jijini DAR ES SALAAM kuwa kamati hiyo iliketi mwezi Oktoba,2017 na kujiridhisha kupitia vigezo vilivyowekwa kuwa Rais MUSEVENI anakidhi vigezo vyote.

Aidha DK.NANGALE amesema Jenerali MUSEVENI anastahili tuzo hii baada ya mwalimu JULIUS NYERERE na KENETH KAUNDA ambao walitunukiwa tuzo hiyo mwaka 2014.

DK.NANGALE amevitaja vigezo vilivyozingatiwa kuwa ni pamoja na mchango wake katika Ukombozi wa UGANDA kutoka tawala dhalimu miaka ya 1970 hadi 1980.

Nyingine ni mchango mkubwa wa kipekee alioutoa katika kusimamia amani katika nchi zilizokumbwa na migogoro ya ndani huko SOMALIA,JAMHURI YA AFRIKA YA KATI,KONGO na BURUNDI.

Mbali na vigezo hivyo DK.NANGALE ameongeza kuwa kigezo kingine ni Rais MUSEVENI amejipambanua kuwa muumini dhabiti wa Umajumuhi wa Afrika.

Tuzo ya Ukombozi Afrika inatambuliwa barani Afrika na Kimataifa lengo lake ni kutambua mchango wa viongozi wa bara la Afrika ,wapigania uhuru,wapatanishi wa Amani na washiriki wengine wa Ukombozi wa Afrika.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments