Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Alhaji Majid Mwanga.

magu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani
Alhaji Majid Mwanga kuwasaka, kuwakamata na kuwa”kisha katika
vyombo vya sheria wafugaji wote wanaodaiwa kuhusika katika
matukio ya kuwashambulia kwa viboko wananchi wa Kijiji cha
Fukayosi kilichopo Wilayani humo.
Mhe. Dkt. Magufuli aliyekuwa akisa”ri kwa gari kutoka Dodoma
kwenda Jijini Dar es Salaam ametoa agizo hilo leo tarehe 17 Machi,
2017 aliposimama katika kijiji hicho baada ya kuona wananchi
wengi wakiwa wamekusanyika kando ya O”si ya Kata.
Baada ya kusimamisha msafara wake, Mhe. Rais Magufuli aliwaita
wananchi waliokuwa wamekusanyika huku wakiwa wameshika
mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kutaka wafugaji wa jamii ya
Wamang’ati waondolewe na kisha akatoa nafasi kwa baadhi yao
kueleza dukuduku lao.
Wananchi hao ambao ni wakulima na mfugaji mmoja aliyejitokeza
wakaeleza kuwa Wamang’ati wamekuwa wakiwanyanyasa kwa
kuingiza mifugo katika mashamba yao ya mazao na wakithubutu
kuwakataza wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi kuuawa.
Katika majibu yake, pamoja na kutaka wote wanaodaiwa
kuwashambulia wananchi kwa viboko wakamatwe Mhe. Rais
Magufuli amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukomesha mara
moja vitendo vya wafugaji kuwapiga wakulima na wakulima
kuwapiga wafugaji, na pia kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha
mifugo yao katika mashamba ya wakulima.
“Kuanzia leo isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima
kumpiga mfugaji wala mfugaji kulisha mifugo yake kwenye
mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia mimi
mwenyewe.
“Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya na Viongozi mlishughulikie hili
kabla mimi sijawashughulikia nyinyi, wale waliopiga watu,
#Sibukamedia

Comments

comments