Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA, DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ameanza ziara mkoani TANGA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA, DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ameanza ziara mkoani TANGA ambapo amesema waliojinufaisha na fedha za ujenzi wa hospitali ya MKATA wajiandae kuzirudisha  au kwenda gerezani.

Rais DKT.MAGUFULI ametoa kauli hiyo aliposimamishwa na wananchi wakati akielekea mkoani TANGA  ambapo anaenda kukutana na Rais wa UGANDA,YOWERI MUSEVEN kwa ajili ya kusaini mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka UGANDA mpaka TANZANIA.

Aidha Rais MAGUFULI ameamuru JKT KABUKU  kurudisha eneo la ekari 50 kwa serikali ya kijiji baada ya kushindwa kuliendeleza kwa muda mrefu tokea wakichukue.

Akizungumzia suala la ukosefu wa maji katika eneo hilo,Rais MAGUFULI amekiri kupokea hoja hiyo kutoka kwa wabunge na viongozi wengine wa wilaya na ameahidi kulishughulikia suala hilo.

Rais DKT.MAGUFULI yuko mjini TANGA kuzindua bomba la mafuta lenye urefu wa zaidi ya kilomita 1425 ambalo litaanzia HOIMA  nchini UGANDA  mpaka CHONGOLEANI,  TANGA ambapo amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia vijana kupata ajira.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments