Rais Magufuli amuapisha Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya kuwa RAS Kagera

apa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 22 Novemba, 2016 amemuapisha Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Hafla ya kuapishwa kwa Kamishna Diwani Athuman Msuya imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene,  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu na Makamishna wa Polisi.

Baada ya kuapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Katibu wa Sekretarieti ya Maadili, Idara ya Viongozi wa Siasa Bw. Waziri Yahaya Kipacha.

Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Amantius Msole ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

22 Novemba, 2016

Comments

comments

Random Posts