Rais John Pombe Magufuli amepongezwa kwa hatua anazochukua kuhakikisha raslimali za taifa zinalindwa.

IMG-20170615-WA0031Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania amepongezwa kwa hatuaa anazochukua katika kuhakikisha rasilimali za Taifa zinalindwa vema na kukuza uchumi wa nchi.

IMG-20170615-WA0032

Hayo yamesemwa leo katika hafla ya kigoda cha mwalimu Nyerere chuo kikuu cha Dar es salaam na Profesa Patrick Lumumba kuwa Rais Magufuli amesimama imara kupigania haki ya wanyonge na kuwa ni kiongozi bora na mfano wa kuigwa barani Afrika.

Aidha Profesa Lumumba amemsifu Rais Magufuli kwa ujasiri mkubwa aliouonyesha katika kupigania masuala ya madini yalipotea kwa kipindi kirefu hadi sasa ambapo ameweza kukaa chini na kukubaliana na wahusika ambao wamekubali kulipa deni hilo.

Profesa Lumumba amepongeza juhudi za baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa juhudi kubwa aliyoifanya katika kulipigania Taifa na kupambana na suala la kukataa kuonewa na kutawaliwa kimabavu ambapo hadi hivi sasa tunajivunia maendeleo ya Afrika.

IMG-20170615-WA0029
Kongamano la siku tatu la Kigoda cha mwalimu limewashirikisha wadau kutoka mataifa mbalimbali katika kuuenzi na kuujadil utamaduni na nafasi za viongozi , wasanii na siasa, katika maendeleo ya Afrika.

Mwandishi : Tuse Kasambala.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts