Rais DKT. JOHN POMBE MAGUFULI amefanya mazungumzo na Rais wa ZANZIBAR

rAIS mAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. JOHN POMBE MAGUFULI amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa ZANZIBAR na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT. ALI MOHAMED SHEIN, Ikulu Jijini DAR ES SALAAM.

Rais MAGUFULI ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais SHEIN ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM ZANZIBAR wamezungumzia masuala mbalimbali yahusuyo chama hicho.

Baada ya mazungumzo hayo Rais SHEIN amesema wamejadili kuhusu kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Wakati huo huo, Rais MAGUFULI amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan hapa nchini MASAHARU YOSHIDA.

Viongozi hao wamezungumzia masuala mbalimbali yahusuyo utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofanywa kwa ushirikiano wa JAPAN na TANZANIA hususani ya ujenzi wa barabara na madaraja.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments