Polisi wawili wauawa katika mlipuko Mogadishu

Maafisa wawili wa Trafiki wameuawa katika mlipuko wa kujitoa muhanga wa gari, uliotokea katika makao makuu ya idara ya trafiki mjini Mogadishu.

Milipuko mikubwa ilisikika katika makao hayo makuu ya Trafiki huko Shangani Mogadishu, na baadaye kufuatia na ufyetuaji risasi.

Wapiganaji wa kundi la al-Shabab wamedai kuhusika.

Katika taarifa yao kundi hilo limedai kwamba shambulio hilo lilipangwa vyema.

Mpiganaji mmoja aliliendesha gari lililokuwa na vilipuzi na mwingine alijaribu kuyavamia makao hayo makuu ya trafiki, lakini alipigwa risasi, Abdifatah Omar Halane, msemaji wa utawala wa mj wa Mogadishu ameliambia AFP.

Mara nyingi Al-Shabab hushambulia maeneo ya jeshi na raia katika kampeni yake ya kuipindua serikali ya Somalia.

Comments

comments