Polisi watafuta sababu ya mauaji Las Vegas

las vegas

Polisi wanajaribu kugundua sababu ya ufyatuaji mkubw wa risasi uliosababisha vifo vya watu 59 na kuwajehi wengine 527 kwenye warsha moja huko Las Vegas.

Mtu mwenye silaha Stephen Paddock, 64, alifyatua risasi kutoka ghorofa ya 32 ya hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwa warsha moja ya mziki Jumapili usiku.

Polisi walipata bunduki 23 kwenye chumba chake cha hoteli na zingine 19 na vilipuzi nyumbani kwake huko Nevada.

Lakini hadi sasa hakuna sababu ya hatua hiyo yake iliyoibuka.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments