Polisi Kilimanjaro walitia mbaroni jambazi sugu

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amesema majira ya saa tatu usiku, majambazi walivamia duka la mfanyabiashara Ibrahim Meena na kumpiga bastola kichwani.

Moshi.  Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia jambazi sugu aliyekuwa akihusika na matukio mbalimbali ya uporaji.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amesema majira ya saa tatu usiku, majambazi walivamia duka la mfanyabiashara Ibrahim Meena na kumpiga bastola kichwani.

Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea maeneo ya Rau River katika Kata ya Kahe Magharibi, lakini polisi walipata taarifa na kufanikiwa kukamata gari lililohusika likiwa na mapanga mawili na nondo.

Amesema wakati tukio hilo walipata taarifa kutoka kwa wananchi na baadaye walifanikiwa kumkamata jambazi huyo sugu aliyekuwa anatikisa Mji wa Moshi.

Kamanda amesema jambazi huyo amekiri kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu akiongoza mtandao wa majambazi mkoani humo.

“Sitataja jina wala idadi ya matukio na gari lililohusika kufanya tukio hilo la uhalifu kwa kuwa ni suala la kiuchunguzi ili kufanikisha kuwakamata majambazi waliohusika,’’amesema.

Comments

comments