Papa Francis alaani vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto


Papa Francis amesema kuwa yupo upande walioathirika zaidi ya 300 waliofanyiwa ukatili wa kingono na baadhi ya makaasisi wa kanisa hilo katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani.

Vatican imesema kuwa inataka kusikiliza kwa kina hoja za wahanga hao ili kujua kwa kina nini kilichotokea dhidi yao kutoka kwa makaasisi hao na kuliita tukio hilo kuwa ni la kinyama.

Hatua hii inakuja baada ya waendesha mashtaka nchini Marekani kubaini kuwa zaidi ya watoto 1,000 huko jimbo la Pennsylvania walifanyiwa ukatili huo.

Askofu wa kanisa Katolik nchini Marekani ameagiza kufanyika uchunguzi ambao utaongozwa na Vatican.Kadnal Daniel DiNardo ambaye ni rais wa kundi la maaskofu ameiita kashfa hiyo kuwa ni matokeo ya kushindwa kuzingatia uongozi wa kidini.

Cardinal DiNardo wa Texas alisema siku ya Alhamis siku mbili baada ya ripoti hiyo kutolewa kwamba kanisa Katoliki kwa sasa linakabiliwa na mgogoro wa kiimani ambapo si kwamba tu unahitaji mazungumzo ya kidini tu bali kuwepo kwa mabadiliko ili kuzuia dhambi hiyo kujirudia na kwamba ripoti hii ni ushahidi tosha.

Amesisitiza kuwa baraza kuu la maaskofu wa Marekani (USCCB),limebainisha maeneo malengo matatu ili kuzia kufanyika ukatili huo na kuwachukulia adhabu kali wale wote watakaobainika kufanya vitendo hivyo.

Baraza hilo la USCCB limesema litapanua uwigo wa namna ya kupokea taarifa za hali inavyoendelea katika dayosisi kuhusiana na ukiukwaji huo.

Askofu huyo pia ametaka ujumbe wa wawakilishi wa Papa kufanya uchunguzi wa kashfa zinazomkabili Kadnal Mstaafu wa Washington DC Theodore McCarrick mwenye umri wa miaka 88 aliyejiuzuru mwezi uliopita.

Papa Francis

Kadnal huyo anatuhumiwa kuwafanyia ukatili huo vijana kadhaa wa kiume akiwepo mmoja aliyekuwa akihudumu kwa karibu na Kadnal huyo miaka 47 iliyopita.Papa Francis alikubali barua ya kujiuzuru kwa Kadnal huyo na kumtaka kuendelea kuomba wakati kanisa linaendelea kushughulikia mashataka yake na kuona ni adhabu gani inamfaa.

Comments

comments