OFISA Mtendaji wa Kijiji cha Jija katika wilaya ya Maswa afikishwa mahakamani.

OFISA Mtendaji wa Kijiji cha Jija katika wilaya ya Maswa mkoani  Simiyu,Tabu Mpina amefikishwa katika Mahakama  wilaya hiyo kwa madai ya wizi wa fedha Sh 3,997,000 za ushuru wa soko huku akiwa Mtumishi wa Serikali.

Imedaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Polisi,Mkaguzi Nassibu Swedy mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Maswa,Tumaini Marwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti katika kipindi cha Mwaka 2016 na 2017 katika kijiji cha Jija.

Mwendesha Mashitaka,Swedy ameieleza mahakama kuwa Mshitakiwa akiwa mtumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa alikuwa na jukumu la kukusanya ushuru katika soko lililopo kijiji hicho na kasha kuziwasilisha kwa Mwajili wake lakini hakufanya hivyo na hatimaye kukamatwa na polisi na kisha kufunguliwa kesi hiyo.

Amesema kuwa mshitakiwa hata alipotakiwa na Mwajili wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuwasilisha kiasi hicho cha fedha alichokuwa amekikusanya kwa kipindi hicho lakini alikuwa akipiga danadana na kushindwa kuziwasilisha. Amendelea kuileza Mahakama hiyo kuwa kosa alilofanya mshitakiwa huyo ni kinyume na kifungu 270 ya sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Mshitakiwa amekana  shitaka lake kuachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na mdhamini mmoja mwenye mali isiyohamishika ambaye atasaini hati hiyo thamani ya Sh Milioni 5 ya maandishi na kesi hiyo itatajwa tena Januari 11 mwakani na upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

#Sibukamedia

Comments

comments