Ndege iliyotoboka shimo kwenye injini yatua salama Australia.

Australia

Ndege moja ya shirika la China Eastern Airlines ililazimika kurudi mjini Sydney Australia baada ya kupatwa na hitilafu wa mitambo ambayo ilisababisha shimo sehemu ya injini ya ndege hiyo.

Ndege ya MU736 ilikuwa safarini kutoka Sydney ikilekea Shanghai China lakini rubani akaripoti kuhusu matatizo kwenyr injini katibu saa moja baada ya ndege kuanza safari.,

Abiria waliambia vyombo vya habari kuwa walihisi harufu na kitu kinachochomeka ndani ya ndege.

Ndege hiyo aina ya Airbus A330 ilitua salama na hakukuwa na ripoti zozote za majeruhi.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts