Naibu Waziri Wanchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, SELEMANI JAFO amezielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa Elimu na Ujuzi kwa wakulima na wafugaji kupitia wataalam mbalimbali ili waweze kuzalisha kwa tija.

SELEMANI JAFO

Naibu Waziri Wanchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, SELEMANI JAFO amezielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa Elimu na Ujuzi kwa wakulima na wafugaji kupitia wataalam mbalimbali ili waweze kuzalisha kwa tija.

Naibu Waziri JAFO amesema hayo wakati akifunga kilele cha Maonesho ya Wakulima na wafugaji NANENANE Kanda ya Kati katika Viwanja vya Nzuguni mijini Dodoma.

Amesema kuwa kupitia wataalamu hao kutasadia Wakulima na Wafugaji kuzalisha mazao kwa wingi ambayo yatatosheleza kwa chakula kwa mwaka mzima na kuvipatia malighafi viwanda vilivyopo nchini.

Aidha amesema  Mamlaka za Serikali za Mitaa ziimarishe na kutumia vituo vya kufundishia wakulima vilivyopo nchini katika maeneo mbalimbali kuwapatia wakulima maarifa na ujuzi katika uzalishaji wenye tija.

Katika hatua nyingine amesema kuwa maeneno ya malisho yatengwe na kuboreshwa   ili kuepuka migongano inayoleta migogoro ya mara kwa mara.

 Wakati huo huo,  Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi WILLIAM Ole NASHA amesema Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya Tabianchi na Uhaba wa malisho ya mifugo na maji.

Ole NASHA ametoa kauli hiyo katika  kilele cha maonesho ya wakulima na wafugaji NANENANE Kanda ya Kati katika Viwanja vya Nzuguni mijini Dodoma, ambapo amesema kuwa kuwepo kwa changamoto hizo kunasababisha kupungua kwa uzalishaji wa mazao.

Ameongeza kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeandaa na kuzindua Muongozo wa Kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi na kusambazwa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya kutumiwa na maafisa Ugani.

Hata hivyo Ole NASHA amesema kuwa maonesho ya Nanenane yamekuwa chachu  kwa wadau wa kilimo na ufugaji kujifunza mbinu za kisasa za kilimo na kuongeza tija katika uzalishaji.

  • Mwandishi : Barnaba Kisengi
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts