Naibu Waziri wa Nishati amewaagiza watendaji wa Tanesco kuhakikisha wanakata umeme kwa sababu maalum.

Naibu Waziri wa Nishati, SUBIRA MGALU amewaagiza watendaji wa Tanesco kuhakikisha wanakata umeme kwa sababu maalum na si kukata hovyo na kuwaletea wananchi adha ya kukosa huduma hiyo.

Naibu Waziri ametoa agizo wakati wa ziara ya kukagua mradi wa TEDAP unaohusu upanuzi na ujenzi wa vituo vya kupozea Umeme na njia za Umeme vya MBAGALA, GONGO LA MBOTO, KIPAWA na CITY CENTRE.

Amesisitiza kuwa Tanesco wanatakiwa kukata Umeme pale inapobidi na kwamba wanapaswa kutoa taarifa ili kuepusha adha kwa wananchi hasa wanaotegemea nishati hiyo kwa ajili ya kuwaingizia kipato.

Aidha, amewaagiza watendaji wa Tanesco wanaosimamia mradi huo wa TEDAP jijini DAR ES SALAAM, kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika tarehe 15 Desemba mwaka huu.

Mradi wa TEDAP unahusisha upanuzi na ujenzi wa Vituo Vipya 19 vya kupoza Umeme wa Msongo wa kV 132/33 na kV 33/11 pamoja na ujenzi wa njia za Umeme wenye Msongo wa kV 132, kV 33 na kV 11 katika Mikoa ya ARUSHA, DAR ES SALAAM na KILIMANJARO na utagharimu Dola milioni 43 zilizotolewa na Benki ya Dunia.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments