Naibu Waziri Ofisi ya Rais ameiagiza mahitaji ya watu wenye Ulemavu Kushugulikiwa.

Naibu  Waziri  Ofisi ya Rais  TAMISEMI, JOSEPH KAKUNDA  ameiagiza mikoa na halmashauri zote nchini  kuhakikisha zinaunda Kamati za kushughulikia mahitaji ya watu wenye Ulemavu katika Kata na Vijiji, kabla ya  June 30, 2018.

Naibu waziri KAKUNDA ametoa agizo hilo wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya mji BARIADI Mkoani SIMIYU.

Amesema Serikali imetenga shilingi milioni 50 kuliwezesha Baraza la wenye Ulemavu Kitaifa kufanya kazi zake kwa mujibu wa Sheria ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Kamati zinaundwa hadi ngazi ya vijiji, ili kufanikisha  azma hiyo,

Aidha ameziagiza Halmashauri zote Nchini kuwapa Kipaumbele Wajasiriamali wenye Ulemavu katika utoaji wa Mikopo inayotokana na asilimia 10 ya Mapato ya ndani ili waweze kupata mitaji ya kuendeshea shughuli zao mbalimbali za ujasiriamali na kujikwamua kiuchumi.

Akisoma risala ya watu wenye ulemavu mwenyekiti wa SHIVYAWATA BI.UMMY NDERININANGA ameiomba serikali kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapatiwa bima za afya, ofisi za SHIVYAWATA,  kuongezwa kwa nafasi za ajira kwa watu wenye ulemavu.

Mengine ni  kutoa mikopo kwa watu wenye ulemavu,kuongeza ulinzi kwa watu wenye ualbino na wanafunzi wa elimu ya juu wenye ulemavu kupewa ruzuku badala ya mikopo, ambayo yote yalitolewa ufafanuzi na Viongozi wa Serikali.

 

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments