Mzee King Majuto, msanii maarufu na mkongwe wa vichekesho Tanzania afariki dunia

sanii mkongwe na maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki Amri Athuman maarufu Mzee Majuto amefariki dunia wakati akipokea matibabu kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo Dar es Salaam Tanzania.

Muigizaji huyo veterani alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya kufariki kwake.

Taarifa ya ikulu imesema King Majuto amefariki dunia majira ya saa 1:30 Jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Tayari watu maarufu ndani na nje ya Tanzania wametuma salamu za rambirambi kwa familia yake kupitia mitandao ya kijamii, miongoni mwao Rais wa Tanzania John Magufuli.

Rais Magufuli amesema King Majuto atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa na wa muda mrefu alioutoa kupitia sanaa ya uigizaji na uchekeshaji, ambapo alishiriki kuelimisha jamii, kuendeleza na kukuza sanaa na kuunga mkono juhudi za chama na Serikali katika kuhimiza maendeleo.

King Majuto alikuwa kielelezo cha safari ndefu ya sanaa kwa nchi yetu, kwa muda wote amedhihirisha kipaji, ujuzi na uwezo wa hali ya juu katika uigizaji na uchekeshaji na hivyo kuwa kipenzi cha Watanzania na wasanii wenzake, hatutasahau ucheshi wake, upendo na uzalendo kwa nchi yake wakati wote wa uhai wake,” amesema Rais Magufuli.

Kiongozi huyo wa nchi alimjulia hali msanii King Majuto alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam 31 Januari, 2018.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, ambaye pia ni mbunge wa Kigoma-Ujiji Zitto Kabwe amesema: “Nimepokea Taarifa ya msiba wa Mzee Majuto kwa masikitiko makubwa sana. Tumshukuru Mola kwa uwezo wake na kuwaombea wafiwa kwa mola awape subra.”

Akiwa kama mfalme wa tasnia ya maigizo ya uchekeshaji nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Mzee Majuto aliweza kujizolea umaarufu mkubwa kupitia namna ambavyo alikua akiigiza na kuwa miongoni mwa watu wenye mvuto mkubwa miongoni mwa wasan

Afya ya Mzee Majuto ilizorota zaidi kuanzia mwaka 2018 ambapo awali alipelekwa nchini India kwa matibabu baada ya Rais wa Tanzania John Magufuli na wapenzi wa sanaa ya Mzee Majuto kumchangia ili kunusuru uhai wake kabla ya baadae kurejea nchini Tanzania.

Wiki chache zilizopita taarifa za uongo za kifo chake zilisambaa mitandaoni kabla ya familia yake kukanusha mara kwa mara.

Majuto aliyezaliwa mkoani Tanga Kaskazini mwa Tanzania mwaka 1948 alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka tisa.

Amecheza kwa mafanikio makubwa kwenye tamthiliya kama vile Mama Nitilie, Kondakta na nyinginezo nyingi zilizompa umaarufu mkubwa.

Kabla ya kifo chake tayari alikwisha wasamehe baadhi ya waandaaji na wasambazaji ambao inasemekana walikua wakimdhulumu mamilioni ya fedha baada ya waziri anayehusika na sanaa nchini Tanzania Harisson Mwakyembe kutishia kuwashitaki watu hao.

Atabaki kuwa nembo ya tasnia ya uigizaji wa vichekesho n

Comments

comments