Mwenyekiti wa mtaa wa BWAWANI aomba wahudumu wa afya kuongezeka.

Mwenyekiti wa mtaa wa BWAWANI A kata ya HOMBOLO manispaa na mkoa wa DODOMA, LIVINGSTON YONA MLUGU ameiomba serikali kuwaongeza wahudumu wa afya katika kituo chao cha afya cha HOMBOLO kutokana na kituo hicho kuwa na upungufu wa wahudumu ili hali uhitaji wa huduma za afya ni mkubwa

MLUGU ametoa ombi hilo wakati akizungumza na Radio Sibuka fm ilipomtembelea ofisini kwake ambapo amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa watu na wingi wa uhitaji wa huduma ya matibabu kumefanya kuwepo kwa upungufu wa madaktari jambo linalosababisha foleni katika kituo chao cha afya

Katika hatua nyingine mwenyekiti mlugu amekiri kutokuwepo kwa dirisha maalumu kwa ajili ya huduma ya watu wenye bima za afya pamoja na wazee kama serikali ilivyo agiza kuwepo kwa madirisha maalumuj kwa ajili ya matibabu ya wazee

  •  #SIBUKAMEDIA

 

 

 

Comments

comments