Mwenyekiti wa kampeni ya Trump ajiuzulu

Mwenyekiti wa kampeni za mgombea wa Republican nchini Marekani Donald Trump, amejiuzulu baada ya ufichuzi kuhusiana na kazi za mwenyekiti huyo Paul Manfort nchini Ukraine.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa baada ya kuwasili Louisiana kujionea uharibifu uliosababishwa na mafuriko jimboni humo, Trump alisema Manafort alijitolea kuachia nafasi yake mapema Ijumaa, na kumtaja kuwa “mweledi wa ukweli.”

“Nimefurahishwa kabisaa na kazi yake kubwa katika kusadia kutufikisha tulipofikia leo, na hususan kazi yake kutuongoza kupita katika mchakato wa kupata wajumbe wa kutuunga mkono katika mkutano mkuu wa chama,” alisema Trump.

Kujiuzulu kwa Manafort kumekuja siku moja baada ya shirika la habari la Associated Press kuripoti kuwa barua pepe za siri kutoka kampuni ya Manafort zilikinzana na madai kwamba hakuwahi kufanya ushawishi kwa niaba ya wanasiasa wa Ukraine nchini Marekani.

#DW

Comments

comments