MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Dodoma Mh.David Mwamfupe ametoa wito kwa waandaaji wa maonyesho ya wakulima na wafugaji Nane nane.

DODOMA

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Dodoma Mh.David Mwamfupe ametoa wito kwa waandaaji wa maonyesho ya wakulima na wafugaji Nane nane Mkoani Dodoma kutathimini na kushirikkisha wahusika wa maonyesho  hayo ambao ni wakulima kutoka vijijini

Mh.Mwamfupe ametoa Rai hiyo alipotembelea mabanda hayo na kueleza kuwa elimu inayotolewa na wataalamu ni kubwa hivyo inabidi kuendelezwa na kuwafikia wakulima moja kwa moja ambapo pia ameshauri maafisa kilimo kujiwekea utaratibu wa kupeleka wakulima kutoka katika halmashauri zao kwenye maonyesho hayo ili kwenda kujifunza zaidi                                                 

Wakizungumza na  fm baadhi ya wakulima walioshiriki katika maonyesho hayo wao wameiomba Serikali kuangalia upya suala la uongezwaji wa muda wa maonyesho hayo ili elimu na utaalamu wanaoutoa uweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa manufaa ya Taifa

Maonyesho ya wakulima Nane nane ni maonyesho ya kumi kufanyika Mkoani Dodoma ambapo kwa mwaka huu yameratibiwa na uongozi wa kanda ya kati huku katika miaka inayofuata yakitarajiwa kuwa yenye tija na kuvutia zaidi.

  • Mwandishi : Barnaba Kisengi
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts