Mshauri wa zamani Michael Flynn akiri kuwahadaa FBI

marekani

Aliyekuwa mshauri mkuu wa masuala ya usalama wa taifa wa Donald Trump, Michael Flynn, amekiri kwamba aliandikisha taarifa ya uongo kwa idara ya uchunguzi wa jinai ya Marekani, FBI, mwezi Januari.

Bw Flynn alishurutishwa kujiuzulu mwezi mmoja baada yake kupotosha ikulu ya White House kuhusu mkutano wake na balozi wa Urusi kabla ya Trump kuingia madarakani.

Mashtaka dhidi yake yaliwasilishwa na mwanasheria maalum Robert Mueller kama sehemu ya uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani wa 2016.

Bw Flynn alifika mahakamani Ijumaa.

Alikiri kosa moja ya kutoa makusudi “taarifa za uongo, za kubuni na za kupotosha”.

Kwa mujibu wa mwanahabari wa AFP, Bw Flynn aliulizwa na Jaji Rudolph Contreras iwapo alitaka kukiri makosa hayo na akajibu kwa kusema “Ndio”.

Jaji aliendelea: “Nakubali kukiri kwako makosa. Hivyo hakutakuwa na kusikizwa kwa kesi na labda huenda kusiwe na rufaa.”

  • #SBUKAMEDIA
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments