Mshauri wa rais Donald Trump ajiuzulu.

QAZ

Travis Kalanick, mkuu wa kampuni ya Uber amejiuzulu katika kundi linalomshauri rais Trump baada ya kukosolewa vibaya na wafanyikazi pamoja na Umma.

Bodi hiyo ambayo pia inamuorodhesha afisa mkuu wa kampuni ya Tesla Elon Musk inatarajiwa kukutana na rais siku ya Ijumaa.

Uber ni miongoni mwa kampuni za teknolojia zilizo na wasiwasi kuhusu athari za marufuku ya uhamiaji kwa nguvu kazi yake.

Kampuni hiyo imesema kuwa imeanzisha hazina ya dola milioni 3 kuwasaidia wale ambao wameathiriwa.

Watu hao ni pamoja na madereva wa Uber.

Hatahivyo Elon ametuma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter akisema atahudhuria mkutano wa Ijumaa.

”Baraza la ushauri hutoa ushauri pekee na kuhudhuria kikao hicho hakumaanishi kwamba ninakubaliana na matendo yake”,alisema.

”Mimi na wengine tutapinga agizo la hivi karibuni la rais kuhusu uhamiaji na kutoa mapendekezo ya mabadiliko yatakayofanyiwa sera hiyo”.

Comments

comments