Msanii maarufu wa filamu za Tanzania (Bongo muvi) Irene Uwoya ametambulishwa rasmi kuwa balozi wa Itel Tanzania.

IMG-20170526-WA0023

Msanii maarufu wa filamu za Tanzania (Bongo muvi) Irene Uwoya ametambulishwa rasmi kuwa balozi wa Itel Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia sasa.

IMG-20170526-WA0029

Akizungumza  leo jijini Dar es salaam meneja masoko Bw. Wolle Fernando amesema kuwa wameamua kufanya makubaliano ya kushirikiana na  Irene Uwoya kwa muda wa mwaka mmoja wakiamini kupitia yeye atawaunganisha Watanzania wote kwa ujumla.

IMG-20170526-WA0026

Meneja huyo amesema kuwa kampuni ya Itel inatarajia ushirikiano baina yao utawezesha jamii kunufaika kwa kupata elimu kupitia bidhaa zake ambapo kwasasa simu ya Itel S.31 imepewa kipaumbele sambamba na kusaidiana katika kuonyesha ukarimu kwa baadhi ya makundi ya jamii yatakayoendeshwa kupitia “Charity event Program”.

IMG-20170526-WA0027

 

Mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano hayo ya kuwa Balozi wa kampuni hiyo Irene Uwoya amewashukuru Itel kwa kumwamini na kuwataka waandishi wa habari na watanzania wote kutumia simu hizo za ITEL 31 kwakuwa zin ubora wa hali ya juu ambapo unaweza kupiga picha hata katika mwanga hafifu.

  • Mwandishi : Tuse Kasambala.
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments