Mourinho: Manchester United hatubahatishi Europa League.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwamba haamini kwamba anacheza kamari kwa kuangazia zaidi ubingwa wa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.

Meneja huyo, ambaye ameamua kuangazia ligi hiyo badala ya kumaliza katika nafasi nne za kwanza Ligi ya Premia, anasema uamuzi wake ni wa busara.

United wanaongoza 1-0 dhidi ya Celta Vigo nusufainali kutoka kwa mechi ya kwanza wanapoelekea kwa mechi ya marudiano leo Alhamisi jioni uwanjani Old Trafford.

Mourinho amesema kuwepo kwa mechi nyingi ambazo klabu yake inahitajika kucheza kumemlazimu kuamua ataangazia wapi.

       #SIBUKAMEDIA

“Kucheza mechi kumi na saba katika wiki saba haiwezekani. Si kamari, ni matokeo tu ya hali ilivyo,” alisema.

Comments

comments