Moto mkubwa wateketeza jengo refu la makazi London.

LONDON

Jengo moja la ghorofa limeshika moto katika barabara ya Latimer, magharibi mwa jiji la London, watu walio shuhudia tukio hilo wanasema,moto huo umeleta mshituko mkubwa hali iliyosababisha baadhi ya watu kushindwa kutoka katika makazi yao.

Taarifa zinadai kuwa baadhi ya watu bado wamekwama ndani ya jengo hilo linalo waka moto.

Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza mwendo wa saa 01:16, saa za Uingereza na karibu wazima 200 wanapambana nao.

Hadi sasa moto huo unaendelea kuunguza jengo hilo vikosi vya uokoaji na zima moto takriban 200 vikiendelea na kazi hiyo.

Idara ya wazima moto jijini London imetuma malori 40 ya kuzima moto huo

  • #SIBUKAMEDIA.
  • #BBC SWAHILI.

Comments

comments

Random Posts