Mmomonyoko wa maadili, Rais Magufuli akemea.

RAIS

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. JOHN POMBE MAGUFULI, amevitaka vyombo vya habari, Taasisi ya TCRA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wazazi kukemea vikali mambo yanayochochea mmomonyoko wa maadili hasa kwa mabinti.

Rais MAGUFULI amesema anachukizwa na tabia  ya watoto wa kike kuonekana nusu uchi

Rais MAGUFULI ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Jumuiya ya Wazazi mjini DODOMA, na kusisitiza kuwa vyombo vya habai hasa televisheni zinapaswa kuangalia vitu wanavyorusha visiharubu maadili.

Licha ya kusema anapenda muziki Rais ameonyesha kuchukizwa na mabinti wanaocheza utupu huku wanaume wakiwa na mavazi ya staha, na kusema kwamba ni aibu kubwa kwa wazazi kuangalia mambo hayo.

Licha ya kusema anapenda muziki Rais ameonyesha kuchukizwa na mabinti wanaocheza utupu huku wanaume wakiwa na mavazi ya staha, na kusema kwamba ni aibu kubwa kwa wazazi kuangalia mambo hayo.

Rais MAGUFULI ameitaka jumuiya hiyo na watu wote kusimamia maadili, huku akivinyooshea mkono vyombo husika vinavyopaswa kushughulika na masuala ya utamaduni wa Mtanzania na kusisitiza kuwa tunapaswa kulinda utamaduni wetu bila kujali vyama .

  • #SIBUKAMEDIA

.

Comments

comments