Mkuu wa Wilaya ya Ubungo amepokea Rasmi mwenge wa Uhuru.

Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mh.Makori Kisare ameupokea rasmi Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh.Hapi mara baada ya Mwenge kumaliza ziara yake katika wilaya ya kinondoni.

Mh.Kisare ameishukuru serikali ya Mh.Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa juhudi mbalimbali za maendeleo ya Taifa katika kukuza uchumi wa Tanzania ya viwanda.

Mwenge huo Wa Uhuru umekagua na kuzindua miradi mbalimbali iliyopo wilaya Ubungo kama kituo cha Huduma na Tiba kwa wagonjwa waishio na Vvu na Ukimwi kilichopo Mbezi ambacho kinatarajiwa kuhudumia watu wapatao elfu kumi mradi huo uliibuliwa na idara ya Afya ya manispaa ya Ubungo.

Mradi huo umegharimu shilingi milioni 155 ambazo zimetolewa kwa msaada wa wafadhili wa Management &Development for Health.(MDC)

Mbali na hayo kiongozi wa mbio za Mwenge alizindua mradi wa madarasa nane yaliyopo katika shule ya Msingi iitwayo Malamba mawili iliyopo katika manispaa hiyo ambayo yamejengwa kwa fedha za serikali zilizogharimu shilingi 136,000,000.

Maeneo mengine yaliyotembelewa na kuwekwa jiwe la msingi ni kituo cha polisi kati Gogoni kilichopo Kibamba ambacho kinakusudiwa kuwa na jumla ya vyumba 13 wananchi wakiwa wamechangia shilingi 53,000,000 na Nssf wamechangia 50,000,000 jumla ikiwa shilingi 103,000,000/=

Akizungumza kiongozi wa mbio za Mwenge Amour Hamad Amour katika uzinduzi wa kituo cha mawasiliano cha mabasi kiitwacho simu 2000 na kituo cha polisi amewataka madereva watumiao kituo hicho kuzingatia idadi ya upakiaji abiria.

Aidha Amour amewataka madereva hao kujiepusha na ulevi pamoja na utumiaji wa mirungi.

Kituo hicho cha mabasi kina uwezo wa kuhudumia mabasi 560 na bajaji kimejengwa kwa pesa za mapato na kugharimu shilingi 2,376,647,991.89.

Mwenge wa uhuru umehitimisha ziara yake mburahati ambapo umetembelea kituo cha zahanati mburahati ambacho kina uwezo wa kuhudumia watu 30,000 waliopo huko na maeneo ya Barafu utagharimu shilingi 84,000,000.00.

Mwandishi : Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA.

Comments

comments