MKUU wa Mkoa wa Dodoma Jordani Rugumbana, azitaka taasisi za umma na binafsi kusajili sehemu zao za kazi.

rugimbana

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Jordani Rugumbana amewataka wamiliki wa taasisi za umma na za binafsi kufuata utaratibu uliowekwa wa kuzisajili sehemu zao za kazi katika taasisi ya wakala wa usalama na afya mahala pa kazi (OSHA).

Lengo la taasisi hizo kujisajili OSHA ni ili zitambulike na kuweza kufikiwa kwa ajili ya ukaguzi, elimu na ushauri kuhusu uimarishaji wa mifumo ya kuwalinda wafanyakazi na mazingira hatarishi ya kazi.

Kwa utaratibu uliopo ni kuwa wamiliki wa sehemu za kazi zao nchini ziwe za umma au za binafsi wanakatiwa kuhakikisha wanasajili sehemu zao za kazi katika taasisi ya OSHA,ili kunufaika na mambo mengi ambayo yanatolewa na OSHA.

Hayo yameelezwa mjini hapa na Deogratius Yinza katibu tawala  msaidizi Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya mkuu huyo wa mkoa wakati wa kufunga mafunzo kwa wajasiriamali wadogo wa manispaa ya Dodoma yaliyoandaliwa na OSHA.

Yinza amesema kuwa mafunzo hayo kwa wajasiriamalihao ambao wengi wao wapo kwenye sekta isiyo rasmi yanalenga kuondoa mwanya wa elimu ya usalama na afya mahala pa kazi uliopo baina ya taasisi na makampuni yaliyo katika sekta rasmi na wazalishaji wadogo  ambao bado hawajafikiwa na mfumo rasmi wa serikali wa kusimamia masuala ya usalama na afya mahala pa kazi.

Kwa pande wake Kaimu Meneja wa OSHA kanda ya kati Eng,Robert Mashinji analipi la kuzingumza kuhusiana na mafunzo hayo ambayo wamekuwa wakiyatoa katika sehemu mbalimbali nchini.

Lakini ni yapi maneno ya washirki wa mafunzo hayo hapa Eglina Mwikombe na Clement John wakapaza sauti zao.

Mafunzo hayo yameshirikisha wajasiriamali wadogo 107 ambao wanahusika na masula na mazingira kutoka manispaa ya dodoma na pia washiriki hao wamewapatia vifaa vya kufanyi kazi, kwa lengo la kujikinga na viashiri hatari katika mahala pa kazi.

  • Mwandishi : Barnaba Kisengi
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts