MKUU wa Mkoa PAUL MAKONDA ametembelea Ofisi za Clouds Media Group kutoa pole.

 

MKUU wa Mkoa wa DAR ES SALAAM,  PAUL MAKONDA ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa DAR ES SALAAM leo ametembelea Ofisi za Clouds Media Group kutoa pole.

MAKONDA amechukua hatua hiyo  siku moja baada ya ofisi hizo kukumbwa na janga la moto uliotokea hapo jana majira ya saa nne asubuhi.

Viongozi wengine wa serikali waliofika ofisini hapo ni Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni, ALLY HAPI na Meya wa Manispaa ya KINONDONI, BENJAMIN SITTA.

Hata hivyo, tayari matangazo ya vituo vya Clouds FM na Clouds TV yamerejea hewani baada ya kupotea siku nzima  jana kutokana na hitilafu ya iliyosababishwa na moto huo ambao chanzo chake hadi sasa hakijajulikana.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments