Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini amekiri picha zinazosambaa mitandaoni.

Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi, ELIUS MWAKALINGA amekiri picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya UDSM yana nyufa ni za majengo hayo.

Mhandisi MWAKALINGA amewaambia waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM kuwa nyufa kutokea kwa majengo marefu ni kitu cha kawaida.

Aidha mhandisi MWAKALINGA amewatoa hofu watanzania na wanafunzi kuwa majengo hayo yamekidhi vigezo vyote na vipimo wakati wa ujenzi wake hivyo nyufa hizo haziwezi kuleta madhara makubwa.

Aidha mhandisi MWAKALINGA ameongeza kuwa kinachoonekana katika jengo hilo ni kitu kinachoitwa common na wala si mpasuko kama inavyoonekana katika picha .

Amesema tayari wameshatembelea jingo hilo na wanafanya utaratibu wa kurekebisha hivyo watu wawe na amani wala wasiwe na hofu.

Jana picha mbalimbali zilisambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha nyufa katika mabweni mapya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DAR ES SALAAM yaliyojengwa na mkandarasi wa ndani na kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.

#SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments