Mkurugenzi mtendaji TACAIDS asema maambukizi yameshuka na mpango wa pima na kuanza dawa wahimizwa.

img-20161228-wa0015

Imekadiriwa kuwa takribani watu 54,000 walikuwa na maambukizi mapya ya virus vya ukimwi(vvu)nchini Tanzania ambapo hivi sasa kiwango hicho kimeshuka kwa wastani wa 20% kati ya mwaka 2010 hadi 2015.

Amebainisha hayo mkurugenzi  mtendaji wa Tacaids Dr.Leonard Maboko alipokuwa akizungumza leo na wanahabari jijini dar es salaam amesema kuwa pamoja na mafanikio hayo ya kushuka kwa maambukizo ya vvu bado kuna makundi na maeneo ambayo kiwango cha maambukizo bado kipo zaidi ya wastani wa kitaifa na kutolea mfano tafiti za viashiria vya vvu/ukimwi na malaria kwa  2011/12

Amesema kuwa kwa upande wa   Tanzania bara mbukizo ya vvu yalikuwa ni 5.3% ambapo wanawake walionekana wameathirika zaidi kwa  6.2% ambapo wanaume ilikuwa no 3.8% Maambukizo ya vvu ni 3.8 ambapo tafiti ilionyesha mkoa wa Njombe uliongoza kwa kiwango kikubwa cha maambukizo kwa 14.8%ikifuatiwa na Iringa 9.1%na Mbeya kwa 9%

Aidha amesema maambukizo mapya yameshuka kwa asilimia 50 miongoni mwa watoto duniani kote ambapo watoto 290,000 wapya waliambukizwa kwa mwaka 2010 wakati mwaka 2015 ni watoto 150,000 tu walioambukizwa vvu na maambukizo kwa watu wazima hayajashuka tangu 2010 Duniani

img-20161228-wa0014

Hata hivyo mkurugenzi wa tacaids Dr.maboko amesema dunia imejiwekea malengo ya kutokomeza ukimwi kama janga hadi ifikapo mwaka 2030 ili kufikia lengo shirika la umoja wa mataifa linaloratibu mapambano dhidi ya ukimwi.

(UNAIDS)limeweka malengo ya muda ya (90-90-90) ikimaanisha watu wote wanaokisiwa kuwa na vvu kujua hali zao ambapo 90 ya pili asilimia 90 watu wote wataobainika na vvu kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya vvu (ARV)mara moja na 90 ya tatu ikimaanisha watu walioanza dawa waweze kuwa na ufubazo endelevu wa virusi vya ukimwi mwilini mwao.

Dr.Maboko ametoa wito kwa wananchi kupima na kuanza dawa kwa mujibu wa shirika la Afya duniani ambalo linazitaka nchi zote kuwaanzishia dawa mara moja pasipo kujali kiwango cha chembembe za kinga( CD4).

Mpango huu unaitwa” Pima na kuanza dawa” ambapo wizara ya Afya imeshatoa waraka wa kuanza mpango huo tangu octoba 2016 ambapo amesema faida zake ni kuepushwa na magonjwa nyemelezi na kupunguza kasi ya maambukizo kwa wenzi wao.

#SIBUKAMEDIA

#Imeandaliwa na Tuse Kasambala

 

Comments

comments