Misri yakanusha habari kuwa mabaki ya ndege yake yamepatikana, na kusema yalikuwa ni makosa ya tafsiri

Dosari za tafsiri ya taarifa iliyotolewa na shirika la ndege la Misri imesababisha mkanganyiko kuhusiana na hatma ya ndege ya shirika hilo iliyopotea.Ofisa wa shirika hilo amesema mkanganyiko huo unaotokana na makosa ya tafsiri toka lugha ya Kiarabu kwenda Kiingereza kwenye akaunti ya facebook ya shirika hilo. Habari kuhusu kuonekana kwa mabaki ya ndege hiyo karibu na kisiwa cha Ugiriki pia zilitolewa kabla, lakini maofisa wa Ugiriki walikanusha habari hiyo.

Idara ya uchunguzi wa ajali za ndege ya Ufaransa imesema itatuma wataalam watatu na mtaalamu kutoka kampuni ya Airbus kutafuta chanzo cha kupotea kwa ndege hiyo.

Ndege hiyo aina ya Airbus iliruka kutoka Paris kuelekea Cairo ikiwa na abiria 66, na ilipokea muda mfupi baada ya kuingia kwenye anga ya Misri.

Comments

comments